ADD THIS

https://www.facebook.com

Jumatano, 28 Septemba 2016

Leicester City washinda mechi Ligi ya Mabingwa Ulaya

Leicester walicharaza Porto bao moja kwa bila mechi yao ya kwanza nyumbani katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya na kuendeleza mwanzo wao mwema katika dimba michuano hiyo mikuu ya Ulaya.
Islam Slimani, ambaye ana sifa nzuri ya kuwafunga Porto alipokuwa akichezea Sporting Lisbon, alifunga bao lake kwa kichwa dakika ya 25 kutokana na krosi ya Riyad Mahrez.
Nguvu mpya wa Porto Jesus Corona alifunga mlingoti kwa kombora lake lakini Leicester walikwamilia uongozi wao na wakaondoka na ushindi.
Slimani alinunuliwa na Leicester £29m siku ya mwisho sokoni. Ana sifa za kuwahangaisha Porto akiwa Sporting Lisbon hivi kwamba alikuwa amepewa jina la utani "the Dragon Slayer" (Mwuaji wa Zimwi)
Leicester wanaongoza Kundi F wakiwa alama mbili mbele ya FC Copenhagen walio nambari mbili.
Klabu hizo mbili zitakutana tarehe 18 Oktoba.
Leicester walioshangaza wengi kwa kushinda ligi kuu Uingereza msimu uliopita, wameanza vibaya msimu Ligi ya Premia, ambapo wameshindwa mechi tatu kati ya sita walizocheza kufikia sasa. Walifungwa mabao manne na Liverpool na Manchester United.Image result for leicester vs porto

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni